Nikki Mbishi soon, kuachia wimbo ambao hautakuwepo kwenye media yoyote ile bali kwenye simu na computer za mashabiki wake.Nikki kupitia ukurasa wake wa facebook amesema, mtu kuipata single hiyo inabidi achangie shilingi 1000, na atapokea oda kupitia comments za ukurasa wake ambapo zoezi hilo anategemea kulianza siku ya jumatatu.
Wimbo huo ambao amaupa jina la "Msuli Tembo Matokea Sungura" unalenga kuwapa moyo watu wote wanaotumia nguvu, akili na jitihada kwa kiasi kikubwa lakini wanachokipata ni kidogo kulinganisha na walichokiwekeza.
0 comments:
Post a Comment